FM Manyara
FM Manyara
28 October 2025, 6:20 pm

Jeshi la polisi mkoani Manyara limesema kuwa limejipanga kuimarisha ulinzi na usalama siku ya uchaguzi mkuu ambao unatarajia kufanyika october 29 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake,kamanda wa jeshi la polisi mkoani Manyara Ahmed Makarani, amesema jeshi la polisi halitomfumbia macho mtu yeyote atakaeonesha viashiria vya uvunjifu wa amani.
Aidha,Amewataka wananchi kupiga kura Kwa amani na utulivu bila kuvunja amani ya nchi , ambapo amesema mpaka Sasa hakuna matukio ambayo yameripotiwa ya uvunjifu wa amani.