FM Manyara

Viongozi wa kimila na viongozi wa dini kushiriki uchaguzi mkuu 2025

27 October 2025, 10:20 am

Baadhi ya viongozi wa kimila na dini wakimsikiliza Mkuu wa wialya ya Babati. Picha na Mwandishi wetu

Wilaya ya babati imeimarisha ulinzi katika kata zote za mkoa wa Manyara na hawatomfumbia macho mtu yeyote atakayeleta fujo siku ya uchaguzi” Mh Emmanuela Kaganda

Na Mzidalfa Zaid

Wazee wa kimila, Machifu, Malaigwanani, na viongozi wa dini wa kata ya Nkaiti wilayani Babati mkoani Manyara, wamewahasa  vijana kushiriki uchaguzi mkuu bila vurugu yeyote kwani tanzania ni nchi ya amani.

Wamesema hayo mbele ya mkuu wa wilaya ya Babati Emmanuela Kaganda alipokuwa amewatembelea wananchi hao katika kijiji cha Minjingu, wamesema wako tayari kupiga kura na watahakikisha amani inakuwepo ifikapo october 29.

Sauti ya viongozi wa kimila na dini

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Babati mkoani Manyara Emmanuela Kaganda, amewataka wananchi kupuuzia taarifa zinazosambaa katika mitandao ya kijamii na kundi la watu wachache ambao hawaitakii mema Tanzania.

Kaganda amesema wilaya ya babati imeimarisha ulinzi katika kata zote za mkoa wa Manyara na hawatomfumbia macho mtu yeyote atakayeleta fujo siku ya uchaguzi huku akiwataka wananchi washiriki uchaguzi mkuu  na kumchagua kiongozi wanaemtaka.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Babati mkoani Manyara Emmanuela Kaganda
Mkuu wa wilaya ya Babati mkoani Manyara Emmanuela Kaganda. Picha na Mwandishi wetu

Nao baadhi ya wananchi wa kata hiyo, wamempongeza mkuu huyo wa wilaya ya Babati kwakuwa karibu na wananchi hao kwani amekuwa akisikiliza na kutatua kero mbalimbali, ambapo wamesema ifikapo october 29 wataenda kupiga kura na kumchagua kiongozi wanaemtaka.

sauti ya wananchi