FM Manyara

Watumishi wa mahakama wahimizwa kutenda haki

24 October 2025, 5:54 pm

Picha ya baadhi ya wajumbe wa kamati ya maadili ya maafisa wa mahakama

Mkuu wa mkoa wa manyara Queen Sendiga amehimiza watumishi wa mahakama kufanya kazi kwa uadilifu, ambapo amesema kwa sasa malalamiko ya kuzilalamikia mahakama yamepungua

Na Mzidalfa Zaid

Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga amewataka wajumbe wa kamati ya maadili ya maafisa wa mahakama kutenda haki kwa masilahi ya taifa na kuzingatia uaminifu kwa kuchunguza tuhuma za ukiukwaji.

Sendiga ametoa kauli hiyo leo katika hafla ya uapisho wa viongozi na wajumbe wa kamati ya maadili ya maafisa wa mahakama ya mkoa na wilaya zote za mkoa wa Manyara, ambapo  amewataka kuzingatia kanuni na taratibu za kisheria.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga

Aidha, amezitaka kamati hizo kuwahimiza watumishi wa mahakama kufanya kazi kwa uadilifu, ambapo amesema kwa sasa malalamiko ya kuzilalamikia mahakama yamepungua kutokana na utendaji mzuri wa mahakama hizo.