FM Manyara
FM Manyara
21 October 2025, 4:52 pm

Mkuu wa mkoa wa manyara, Queen Sendiga, amewaonya wananchi mkoani Manyara kuepuka vitendo vyovyote vinayoashiria vurugu, uchochezi au uvunjifu wa amani kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika oktoba 29 mwaka huu.
Na Mzidalfa Zaid
Sendiga ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake ,amesema kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa imejipanga kuhakikisha ulinzi unaimarishwa siku hiyo ya kupiga kura.
Aidha,amewaonya watumiaji wa mitandao ya kijamii, hususani kwenye makundi ya whatsapp, kuepuka kusambaza taarifa za uchochezi kwani timu ya mkoa itakuwa na wawakilishi katika makundi hayo watakaokuja wanafatilia taarifa mbalibali.