FM Manyara
FM Manyara
20 October 2025, 4:35 pm

Mkuu wa wilaya ya babati Emmanuela kaganda amewataka wananchi kujitokeza October 29 kupiga kura na kumchagua Kiongozi wanaemtaka atakaeleta maendeleo amani na utulivu.
Na Mzidalfa Zaid
Kaganda ametoa kauli hiyo Leo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, amesema kila mwananchi ana haki ya kupiga kura hivyo ulinzi na usalama utaimarishwa katika maeneo yote ya wilaya ya Babati.
Amewaonya wananchi wote watakaojaribu kuharibu uchaguzi kwani ni kosa kisheria Kwa mtu yeyote kufanya fujo kati zoezi Zima la upigaji kura, hivyo kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya imejipanga kuhakikisha usalama unakuwepo.