FM Manyara
FM Manyara
20 October 2025, 10:38 am

Wananchi wa kata ya Qash na Vitongoji vyake iliyopo Wilayani Babati mkoani Manyara wameahidiwa maji safi na salama pamoja na ujenzi wa Barabara itakayounganisha maeneo mbali mbali ya kata hiyo na Kata nyingine za jirani.
Hayo yamebainishwa na mgombea ubunge wa jimbo la uchaguzi la Babati Vijijini kupitia chama cha mapinduzi Daniel Baran Sillo wakati akizungumza na wananchi wa kata Qash waliojitokeza kusikiliza ilani ya uchaguzi katika mkutano wa hadhara.
Kwa upande wake mgombea udiwani wa kata hiyo Mohamed Issa amesema iwapo atapata ridhaa ya wananchi atashirikiana na mbunge kutatua kero zilizopo kwenye kata hiyo ikiwemo ukosefu wa maji safi na salama, Barabara na umeme kwa baadhi ya Vitongoji kwenye kata ya Qash.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Babati Jackson Haibey ameendelea kuwasisitiza wananchi wa kata hiyo kujitokeza kupiga kura hapo October 29 mwaka huu kwani ni haki yao kikatiba.
Sauti ya Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Babati
