FM Manyara
FM Manyara
11 October 2025, 6:38 pm

Na Emmy Peter
Naibu Waziri wa mambo ya ndani ya Nchi Daniel Sillo na mwenyekiti wa baraza la taifa la usalama barabarani amezindua mfumo mpya wa kielektroniki wa ukaguzi wa vyombo vya moto na utoaji wa stika za usalama barabarani, hatua inayolenga kuimarisha usalama na kupunguza ajali barabarani nchini kwa ubovu wa vyombo vya moto.
Uzinduzi huo umefanyika katika wiki ya nenda kwa usalama barabarani leo mkoani Manyara oktoba 11, 2025 katika ukumbi wa White Rose mkoani hapa ambapo mfumo huo unatarajiwa kuondoa changamoto zilizokuwa zikijitokeza katika ukaguzi wa magari kwa kutumia stika za karatasi, na badala yake kurahisisha huduma kwa njia ya kidigitali.
Kwa upande wake Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani SACP William Mkonda amesema hali ya usalama barabraniinaendelea kuimarika kutokana na juhudi kubwa zinazofanywa na baraza kupitia kikosi cha usalama bararani nchini kutoa elimu ya usalama barabarani usiku na mchana.
Kwa upande wao madereva usafirishaji mkoani Manyara wamekishukuru kikosi cha usalama bara barani kwa kuleta mfumo huo ambapo wameomba mfumo huo kuwa rafik kwa wasiyo kuwa na simu janjaa.
Kaulimbiu ya wiki ya nenda kwa usalama bara barani mwaka huuu inasema “familia yako inakusubiri zingatia usalama”.
