FM Manyara

Serikali kusafisha ziwa Babati

4 October 2025, 6:29 pm

Picha ya Mgombea Urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dokta Samia Suluhu Hassan

Mgombea Urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dokta Samia Suluhu Hassan amesema  serikali imetenga fedha ya kununua Mitambo ya kuondoa Magugu kwenye maziwa likiwemo ziwa Babati.

Na Mzidalfa Zaid

Amesema hayo Leo wakati akihitimisha kampeini zake mkoani Manyara katika viwanja vya stendi ya zamani, amesema lengo ni kuhakikisha maziwa yote yanakuwa masafi na kuanza kutumika katika shughuli ya uvuvi na utalii.

Amesema endapo atapewa ridhaa ya kuongoza Kwa miaka miatano ijayo atanunua boti katika mkoa wa Manyara ikiwemo boti ya usalama na boti tatu zitasaidia katika shughuli za uvuvi.

Sauti ya Dokta Samia Suluhu Hassan

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama Cha mapinduzi CCM Mkoa wa Manyara Peter Toima, amesema wanatarajia kushinda Kwa kishindo katika kata zote 142 zilizopo Mkoani Manyara,kutokana na kazi kubwa ya kukuza uchumi wa Taifa  ambayo imefanywa na Dokta Samia.

Sauti ya Mwenyekiti CCM Manyara Peter Toima