FM Manyara
FM Manyara
19 September 2025, 12:09 pm

Kufuatia malalamiko ya Babigumira Sauli, raia wa Uganda, dhidi ya Shule ya Aldersgate,Babati mkoani Manyara akidai mafao yake kwa kipindi alichokuwa akifanya kazi shuleni hapo, hatimae amelipwa stahiki zake zote.
Na Mzidalfa Zaid
Akizungumza mara baada ya kulipwa fedha hizo amesema fedha zote alizokuwa akizidai amelipwa Sauli ameshukuru mkuu wa mkoa wa manyara Queen Sendiga kwa kusaidia kufanikisha kupata haki yake.
Akiongea kwa niaba ya shule ya Aldersgate, mwakilishi wa shule hiyo Jacob Simba, amesema maagizo yaliyotolewa na mkuu wa mkoa wa Manyara wameyatekeleza kwa muda mfupi kwa kumlipa mwalimu huyo.
Aidha Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga amewataka wamiliki wa taasisi binafsi kuhakikisha wanalipa wafanyakazi wao mishahara na mafao kwa mujibu wa mikataba ya ajira, akisisitiza kuwa serikali haitavumilia unyanyasaji wa aina yoyote kazini.