FM Manyara
FM Manyara
16 September 2025, 6:38 pm

Mkuu wa wilaya ya Babati Emmanuela Kaganda leo amesikiliza na kutatua kero za wananchi ambapo amewataka wakuu wa idara kutenda haki wanapotatua kero za wananchi.
Na Mzidalfa Zaid
Akizungumza katika viwanja vya stendi ya zamani, Kaganda amesema kazi ya serikali ni kutengeneza mazingira wezeshi ili wananchi waishi kwa amani na utulivu wakiwa wanshiriki shughuli za maendeleo bila kuonewa.
Katika kikao hicho baadhi ya wananchi waliojitokeza katika viwanja hivyo wamelezea kero zao ikiwemo kero ya kudai malipo kutokana na kazi za serikali ambazo walizifanya na hawakupewa stahiki zao, ambapo mwananachi mmoja amedai fedha alizotengeneza madawati ya shule huku mwananchi mwingine akimdai mkandarasi ambae alikabidhiwa mradi wa REA.

Kufuatia malalamiko hayo, mkuu huyo wa wilaya, ametoa maagizo kwa viongozi husika kuhakisha walalamikaji hao wanapewa stahiki zao na makabidhiano ya pesa hizo yafanyike katika ofisi ya mkuu wa wilaya.
Aidha, amesema kutakuwa na mwendelezo wa usikilizaji wa kero za wananchi katika maeneo mbali mbali ya wilaya ya Babati na kesho ataendelea kusikiliza kero za wananachi katika stendi ya zamani.