FM Manyara

Manyara kudhibiti ukondefu

14 September 2025, 8:59 am

Picha ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara

Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga amewataka maafisa lishe kukomesha tatizo la ukondefu mkali na utapiamlo Kwa kuifikia jamii na kutoa elimu Ili kudhibiti tatizo Hilo.

Na Mzidalfa Zaid

Sendiga ametoa kauli hiyo Leo katika kikao Cha tathimini ya hali ya lishe, amesema Kwa kipindi Cha mwaka 2024 Hadi 2025 jumla ya watoto 1866 wamezaliwa wakiwa na uzito mdogo.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara

Kwa upande wake afisa lishe mkoa wa Manyara January Darushi amesema hali ya ukondefu Kwa watoto  imepungua kutoka watoto 21,000 hadi 2235, na watoto wenye ukondefu mkali kutoka 474 Hadi 339.

Sauti ya afisa lishe mkoa wa Manyara
Picha ya afisa lishe mkoa wa Manyara

Aidha, afisa lishe wilaya ya kiteto Beatrice Lutanjuka amesema katika kuendeleza lishe mashuleni wameanzisha mradi wa ufugaji sungura mashuleni Ili wanafunzi watumie kama kitoweo na kuwasaidia kupata protini.

Sauti ya afisa lishe wilaya ya kiteto