FM Manyara
FM Manyara
11 September 2025, 9:38 pm

Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga,amewaonya viongozi wa sekta binafsi ambao wamekuwa wakijifanya miungu watu kuacha tabia ya kuwanyanyasa wafanyakazi ikiwemo kutowapatia mikataba
Na Mwandishi wetu
Sendinga amesema hayo Leo katika kikao Cha kusikiliza na kutatua kero za wananchi, ambapo miongoni mwa kero iliyowasilishwa ni baadhi ya waliokuwa walimu wa shule ya Aldersgate kudai mafao yao ambayo waliyatumikia kwa kipindi walichofanya kazi shuleni hapo.
Awali baadhi ya walimu akiwemo aliyekuwa mkuu wa shule hiyo ambae amefanya kazi Kwa kipindi Cha zaidi ya miaka 15, wamesema licha ya kufanya kazi Kwa kipindi hicho hawajawakewa mafao yao baada ya kustaafu ambapo wameiomba serikali iwasaidie kwakuwa waliondolewa shuleni hapo bila utaratibu.
Awali baadhi ya viongozi wa shule hiyo, wamesema malalamiko hayo sio ya kweli kwani walimu hao walikuwa wakijitolea.
Aidha , kufuatia malalamiko hayo , Sendiga amemuagiza kaimu katibu tawala wa mkoa wa Manyara kufuatilia nyaraka shuleni hapo ili achukue hatua zaidi za kisheria.