FM Manyara
FM Manyara
11 September 2025, 9:43 am

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Cuthbert Sendiga amesikiliza na kutatua kero za wananchi kutoka wilaya zote za Mkoa wa Manyara katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Na Mzidalfa Zaid
Katika kikao hicho Sendiga amesikiliza kesi mbali mbali ikiwemo kesi ya mzee aliyefahamika kwa jina la Mandoo ambae alifika ofisini hapo kumlalamikia askari wa jeshi la polisi aliyedaiwa kumsukuma mzee huyo wakati akimpeleka katikaMahabusu ya mahakama baada ya kupewa maagizo na hakimu.
Baada ya kusikiliza kesi hiyo Sendiga amemtaka mzee huyo aseme msaada anaotaka serikali imsaidie ambapo mzee huyo ameiomba serikali imsaidie gharama za matibabu pamoja na kununuliwa supu ambapo mkuu wa mkoa amemkabidhi kiasi cha shilingi laki mbili na kutoa oda ya mzee huyo kununuliwa supu yeye pamoja na marafiki zake.
Mzee Mandoo amemshukuru mkuu wa mkoa wa Manyara kwa moyo wake wa dhati wa kuwasaidia wanyonge ambapo amewataka viongozi wengine kuiga mfano wa kiongozi huyo.
Aidha, katika hatua nyingine sendiga amesikiliza na kutatua kesi mbalimbali ikiwemo migogoro ya ardhi, migogoro ya kifamilia, mirathi na ametoa maagizo ya kesi hizo kutatuliwa ndani ya muda mfupi.