FM Manyara
FM Manyara
2 September 2025, 6:22 pm

Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga amewataka wananchi mkoani Manyara kuzitumia shule za elimu ya watu wazima kwa kujiendeleza kielimu.
Na Mzidalfa Zaid
Sendiga amesema hayo baada ya kagua na kuweka jiwe la msingi katika jengo la elimu ya watu wazima lenye thamani ya shilingi bilioni 400 amesema serikali ya awamu ya sita imetenga fedha hizo kutengeneza mazingira rafiki ya watu wazima kujisomea kwa muda wanaoutaka.
Kwa upande wake afisa elimu ya watu wazima mkoa wa Manyara Ibrahim Mbogo, pamoja na mkufunzi wa Taasisi ya elimu ya watu wazima Emanuel Geydan, wamesema jengo hilo litatoa fursa kwa wananchi wa Manyara kupata elimu ya watu wazima huku wakiitaka jamii kufika katika viwanja vya stendi ya zamani na kupata elimu zaidi.
Nao baadhi ya wanafunzi wanufaika wa mpango huo wa elimu ya watu wazima wamesema wanaishukuru serikali kwa kuanzisha elimu kwa wanafunzi ambao walikatiza masomo kutokana na sabababu mbalimbali ili watimize ndoto zao.
Katika maadhimisho hayo yanayoendelea katika viwanja vya stendi ya zamani, wajasiriamali pamoja na Taasisi mbalimbali zimepata fursa ya kuonesha kazi wanazoifanya, ambapo wamesema maadhimisho hayo yamewasadia kutangaza biashara zao.