FM Manyara
FM Manyara
23 August 2025, 10:41 pm

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Manyara imewataka wagombea nafasi mbalimbali za uongozi kutotoa rushwa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.
Na Mzidalfa Zaid
Hayo yameelezewa leo na afisa TAKUKURU mkoa wa Manyara Hamis Mwinyi, amesema katika kipindi cha uchaguzi kumekuwepo na changamoto ya wagombea kutumia nguvu ya rushwa kwa kutoa zawadi au pesa ili wachanguliwe ambapo wataka wagombea wote kutojihusisha na vitendo vya rushwa.
Kwa upande wake afisa TAKUKURU mkoa wa Manyara Theresia Mallya, amesema athari za rushwa katika kipindi cha uchaguzi ni pamoja na kuchagua viongozi ambao hawana sifa, kudumaza demokrasia na kuondoa uhuru wa wapiga kura.
Aidha, amewataka wananchi mkoani Manyara kutoa taarifa TAKUKURU watakapobaini uwepo wa viashiria vya rushwa katika kipindi chote cha kabla, wakati na baada ya uchaguzi.