FM Manyara

TMDA yabaini uwepo wa bidhaa bandia ya dettol za maji

17 August 2025, 12:22 pm

Picha ya bidhaa bandia ya Dettol za maji

Mamlaka ya dawa na vifaa tiba (TMDA)imebaini uwepo wa bidhaa ya Dettol za maji bandia zinazotengenezwa kinyume cha sheria kwa njia haramu na kubandikwa lebo kuonesha ni dettol zilizo halisi.

Na Mzidalfa Zaid

Akizungumza na Fm Manyara, Meneja wa TMDA Kanda ya kaskazini Proches Patrick amesema utengenezaji wa Dettol hizo bandia umebainika, kufuatia taarifa za kiintelijensia zilizokusanywa na TMDA na kubaini uwepo wa bidhaa hizo na kuwataka wananchi mkoani Manyara kuepuka bidhaa hizo.

Sauti ya Meneja wa TMDA Kanda ya kaskazini Proches Patrick

Amesema bidhaa hizo zilikutwa kwenye nyumba ya kulala wageni iliyopo mkoani Shinyanga ambapo kulikutwa malighafi mbalimbali katika chumba kimojawapo walichokuwa wanaishi raia wawili kutoka nchi jirani ambao wanatuhumiwa kushiriki katikauhalifu huo.

Aidha, amewataka wafanyabiashara mkoani Manyara wanaojihusisha na ununuzi wa bidhaa hizo kununua katika vyanzo halisi na kupewa risiti, huku akitoa onyo kwa watu wanaojihusisha na utengenezaji ,usambazaji au uuzaji wa dawa  bandia.