FM Manyara
FM Manyara
20 July 2025, 8:25 pm

Waumini wa dhehebu la Kanisa la Mungu Tanzania wametakiwa kushiriki uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika october mwaka huu kwa amani na utulivu na kumchagua kiongozi mwenye sifa ya kuongoza.
Na Mzidalfa Zaid
Wito huo umetolewa na Profesa Pastory Majembe ambae ni mchungaji mwandamizi wa Kanisa la Mungu Tanzania alipokuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 65 katika shule ya Kalamu Centla School of Theolgy yaliyofanyika wilayani Babati mkoani Manyara na kuhudhuriwa na waumini wa dhehebu hilo kutoka maeneo mabalimbali ya nchi.
Kwa upande wake Askofu mkuu wa Kanisa la Mungu Tanzania Stephano Sanka, amewataka wahitimu hao kutekeleza yale yote waliyofundishwa shuleni, na kueneza neno la mungu katika makanisa watakayopangiwa kufanya kazi ya kumtumikia Mungu.
Mkuu wa shule hiyo Boniface Majengo ,amewataka watu wote wenye wito wa kumtumikia mungu wafike shuleni hapo ili wapate elimu bora, kwakuwa shule hiyo ina walimu wanaofundisha namna ya kumtumikia Mungu.
Nao baadhi ya wahitimu , wamesema kwa kipindi cha miaka mitatu wamejifunza mambo mengi yatakayowasaidia katika maisha yao ikimwemo kumjua Mungu.