FM Manyara
FM Manyara
11 July 2025, 10:53 pm

Wafanya biashara wa dawa za mifugo mkoani Manyara wametakiwa kuacha Tabia ya kuuza dawa hizo katika minada au sehemu ambayo haitambuliwi na serikali kwani dawa hizo zinakuwa zimepoteza ubora na ufanisi.
Na Mzidalfa Zaid
Wito huo umetolewa Leo na afisa Elimu Kwa umma na huduma Kwa wateja kutoka Mamlaka ya dawa na vifaa Tiba(TMDA) Kanda ya kaskazini Augustino Malamsha wakati akiongea na fm Manyara, amesema dawa za mifugo na dawa na binadamu zinauzwa sehemu ambazo zimethibitishwa kuuza bidhaa hizo.
Kwa upande wake mkaguzi wa dawa kutoka TMDA Kanda ya kaskazini Benson Mcheza , amewataka wafanyabiashara wa dawa kuzingatia Sheria zilizowekwa Kwa kuhakikisha kabla dawa hizo hazijaingia sokoni zinathibitishwa.
Aidha, amewataka wananchi kutoa taarifa TMDA wanapobaini uwepo wa wafanyabiashara wa dawa ambao hawana vigezo vya kuuza dawa , ambapo amesema TMDA inaendelea na ukaguzi wa kuwabaini wafanyabiashara wa namna hiyo.