FM Manyara

Mwenge wa uhuru kukagua miradi 8 Babati mji

2 July 2025, 6:58 pm

Picha ya mwenge wa uhuru

Jumla ya miradi nane yenye thamani ya sh Bilion 3.29 inatarajiwa kukaguliwa na kuwekewa mawe ya msingi wakati wa mbio za mwenge wa uhuru kwenye halmashauri ya mji wa Babati mkoani Manyara ambapo utakimbizwa julai 15 mwaka huu.

Na Mzidalfa Zaid

Akiongea na fm Manyara,Mratibu wa mbio hizo za mwenge Halmashauri ya mji wa Babati Mwalimu Martin Petro ameitaja miradi hiyo itakayowekewa mawe ya msingi kwenye mbio hizo  za mwenge wa uhuru.

Sauti ya Mratibu wa mbio za mwenge Halmashauri ya mji wa Babati Mwalimu Martin Petro

Aidha Mratibu wa mbio za mwenge amesema mpaka sasa miradi yote itakayopitiwa na mwenge wa uhuru inaendelea kukamilika ikiwa ni asilimia 85 na hadi kufikikia siku hiyo ya julai 15 itakuwa imekamilika kwa asilimia mia moja.