FM Manyara

NSSF Manyara yatoa siku 14 kwa waajiri wadaiwa sugu

16 June 2025, 11:43 pm

Picha ya afisa matekelezo mkuu wa mkoa wa Manyara Amina Kassim

Mfuko wa Taifa wa hifadhi ya jamii(NSSF)mkoa wa Manyara unatarajia kuanzisha operesheni maalumu ya ukusanyaji wa madeni kwa waajiri wenye malimbikizo ya michango ili kuhakikisha haki za msingi za wananchama zinalindwa

Na Mzidalfa Zaid

Waajiri wenye malimbikizo ya michango ya wanachama wa NSSF  wametakiwa kuhakikisha wanalipa madeni yote wanayodaiwa na  NSSF ili kuhakikisha haki za msingi za wananchama zinalindwa.

Hayo yamebainishwa na afisa matekelezo mkuu wa mkoa wa Manyara Amina Kassim wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake amesema operesheni hii itahusisha wilaya zote za mkoa wa Manyara.

Amesema watafanya ufatiliaji wa karibu kupitia barua zote za madai, ziara za ukaguzi na mahojiano ya kikaguzi kwa waajiri wote waliobainika na madeni, ambapo mpaka sasa waajiri 100 kati ya 559 wanadaiwa.

Sauti ya afisa matekelezo mkuu wa mkoa wa Manyara Amina Kassim

Aidha, amesema NSSF inatoa wito kwa waajiri wote wanaodaiwa kufika katika ofisi za NSSF ndani ya siku 14 na kuweka utaratibu wa ulipaji wa madeni kabla hatua za kisheria hazijaanza kuchukuliwa.