FM Manyara
FM Manyara
27 May 2025, 12:42 pm

Serikali mkoani Manyara imesema mfumo wa E-RITA unamuwezesha mwananchi kujisajili kwa kiidigital na kurahisisha kupata cheti cha kuzaliwa kwa haraka tofauti na ilivyokuwa awali.
Na Mzidalfa Zaid
Wananchi mkoani Manyara wametakiwa kujisajili kwenye mfumo E-Rita ambao utamuwezesha mwananchi kujisajili kwenye mfumo kupitia njia ya mtandao ikiwemo simu au compyuter.
Wito huo umetolewa na msajili wa vizazi na vifo wilya ya Babati ambaye pia ni mratibu wa wilaya za mkoa wa Manyara Honest Themba wakati akiongea na Fm Manyara, amesema wanaendelea kutoa elimu hiyo kupitia mikusanyiko ya watu ili watu wajisajili kupitia njia ya mtandao.
kwa upande wake msajili msaidizi kutoka ofisi ya Rita wilaya ya Babati Samson Palangyo, amesema ili mwananchi ajisajili anatakiwa kufuata taratibu zote za usajili kwenye mfumo.