FM Manyara
FM Manyara
12 May 2025, 2:16 pm

Mkuu wa Wilaya ya Babati amezungumza na wananchi wa kata ya Galapo juu ya vitendo vya kihalifu hususani ukatili, huku akiahidi kuanza operesheni maalumu akishirikiana na dawati la jinsia kukomesha vitendo hivyo ambavyo si vya kiungwana na vyakujirudia mara kwa mara.
Na Mzidalifa Zaid
Mkuu wa Wilaya ya Babati Emmanuela Mtatifikolo Kaganda, ametangaza kuanza kwa oparesheni maalumu dhidi ya makundi yote ya kihalifu, hususan yanayohujihusha na vitendo vya ukatili katika jamii.
Kaganda ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Galapo katika mkutano wa hadhara, amesema oparesheni hiyo inalenga kutekeleza kikamilifu ajenda kuu aliyoiasisi tangu alipowasili wilayani Babati ya “Amani na maendeleo.”
Kwa upande wa viongozi kutoka dawati la jinsia na watoto wamewataka wananchi kukemea na kutoka taarifa za ukatili wa kijinsia, pale wanapoona unatendeka au kutokea na namna ya kutambua viashiria vya ukatili, na umuhimu wa kuripoti mapema kwa mamlaka husika.