FM Manyara

Jeshi la Zima moto Manyara laadhimisha kilele Cha wiki ya Zima moto

2 May 2025, 11:20 pm

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Manyara, limewataka Wananchi mkoani Manyara kuhakikisha wanatoa taarifa sahihi wanapokumbwa na majanga ya moto au kuzama maji Ili kurahisisha jeshi Hilo kufanya maokozi Kwa wakati.

Na Mzidalfa Zaid

Hayo yameelezwa leo na Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Manyara, Gilbert Mvungi, katika maadhimisho ya Wiki ya Zimamoto Duniani ambayo kimkoa yamefanyika Wilaya Babati mkoani Manyara.

Amesema Katika maadhimisho hayo kumefanyika shughuli mbalimbali za kijamii na utoaji wa elimu kwa wananchi.

Aidha Kamanda Mvungi amesema Kwa kipindi Cha hivi karibuni kumetokea matukio mbalimbali ya watu kufariki Kwa kuzama maji ambapo amewataka wananchi kuchukua taadhari katika kipindi hiki Cha mvua.

Sauti ya kamanda wa Jeshi la Zima moto na uokoaji mkoa wa Manyara