FM Manyara
FM Manyara
30 April 2025, 7:34 pm

Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga amemwagiza katibu tawala wa mkoa wa Manyara kupita kwenye ofisi za umma na binafsi nakukagua mikataba kwa wasio na mikataba ili kuchukua hatua kwa waaajiri wanaokwenda kinyume na sheria za kazi hapa nchini
Na Marino Kawishe
Waajiri katika sekta binafsi mkoani Manyara wametakiwa kuweka mazingira bora ya kazi ikiwa ni pamoja na kuwapatia mikataba wafanyakazi wao na kutatua changamoto mbali mbali zinazowakabili.
Akisoma risala mbele ya mgeni rasmi kwenye siku ya wafanyakazi duniani mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga, katibu wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi mkoani Manyara TUCTA Juma Makanyaga amesema kwenye sekta binafsi ndiko kwenye hali mbaya zaidi.
Akijibu risala hiyo mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga amemwagiza katibu tawala wa mkoa wa Manyara kupita kwenye ofisi za umma na binafsi nakukagua mikataba kwa wasio na mikataba ili kuchukua hatua kwa waaajiri wanaokwenda kinyume na sheria za kazi hapa nchini.

Aidha, baadhi ya wadau mbalimbali wameiomba serikali kuongez amishahara kwa wafanyakazi ili kuboresha maisha ya wafanyakazi.