

11 April 2025, 6:52 pm
Dereva wa boda ameuwawa na watuwasiojulikana kwa kupigwa na kitu chenye ncha kali maeneo ya kichwani na mwili wake kutelekezwa katika eneo la ofisi ya mashataka lilipo mtaa wa Negamsi mjini Babati mkoani Manyara
Na George Agustino
Kijana aliyefahika kwa jina la Kenedy anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 28 hadi 30 ameuwawa na watuwasiojulikana kwa kupigwa na kitu chenye ncha kali maeneo ya kichwani na mwili wake kutelekezwa katika eneo la ofisi ya mashataka lilipo mtaa wa Negamsi mjini Babati mkoani Manyara.
Wakizungumza na fm Manyara baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wamesema tukio hilo limetoke usiku wa kuamkia leo april 11.2025 na kijana huyo ni dereva wa pikipiki maarufu boda boda aliyekuwa akifanyakazi katika kijiwe cha eneo la kanisa la mungu mjini Babati mkoani Manyara.
Kwa upande wake Afisa habari wa maafisa usafirishaji Boda boda Paulo Jamesameliomba jeshi la polisi kushirikiana na madereva wa boda boda kukomesha vijana wanaotoka maeneo mengine kuja mjini wa babati kufanya uhalifu na amewataka madereva bodaboda wenzake kuacha tama ya fedha kwa kuwabeba watu wasio wajua na kuwapeleka umbali mrefu nyakati za usiku.