

11 April 2025, 3:30 pm
Mfanyabiashara mkoani Manyara akutwa ndani ya nyumba yake amefariki baada ya kudaiwa kuuawa kikatili na watu wasiojulikana kwa kuchinjwa nakitu chenye ncha kali.
Na Mzidalfa Zaid
Mfanyabiashara maarufu wilayani Babati mkoani Manyara, Thomas Karatu (48), ameuawa kikatili kwa kuchinjwa na mwili wake umekutwa ndani ya nyumba yake katika kata ya Gendi mkoani Manyara.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wamesema tukio hilo limetokea April 11 2025 katika mtaa wa Gendi Barazani, ambapo mwili wa mfanyabiashara huyo umekutwa ndani ya nyumba yake baada ya kudaiwa kuuawa kikatili na watu wasiojulikana kwa kuchinjwa nakitu chenye ncha kali.
Aidha, Fm Manyara imemtafuta kamanda wa jeshi la polisi mkoani Manyara Ahmed Makarani ili kuthibitisha tukio hilo ambapo simu yake imeita bila mafaniki na juhudi zakumtafuta zinaendelea ili kuthibitisha tukio hilo.