

11 April 2025, 1:12 pm
Viongozi wa halmashauri za mkoa wa Manyara watakiwa kuhamasisha wananchi kujitokeza kuulaki mwenge wa uhuru na kufika katika miradi yote itakayopitiwa na mwenge
Na Mzidalfa Zaid
Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Cuthbert Sendiga amesema mwenge wa uhuru kwa mkoa wa Manyara unaotarajiwa kukimbizwa kuanzia tarehe 12 hadi 18 julai mwaka huu katika halmashauri zote za mkoa wa Manyara.
Sendiga ameyasema hayo katika kikao lilichowakutanisha viongozi, wataalamu, na wadau mbalimbali kutoka halmashauri zote za mkoa wa Manyara, ambapo amesema maandalizi yote ya kuupokea na kuukimbiza mwenge wa uhuru yamekamilika.
Aidha, Sendiga amewataka viongozi kutoka halmashauri zote za mkoa wa Manyara kuongeza hamasa kwa wananchi kujitokeza kuulaki mwenge wa uhuru na kufika katika miradi yote itakayopitiwa na mwenge wa uhuru.