FM Manyara

Takukuru yabaini mianya ya rushwa Babati

27 March 2025, 9:20 pm

Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Manyara Bahati Haule amesema Takukuru imebaini mianya ya rushwa ikiwemo uwezo mdogo wa Halmashauri kumudu jukumu la uondoshaji wa taka ikiwemo taka ngumu.

Na George Agustino

Taasisi ya na Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) Mkoa wa Manyara imefanya uchambuzi wa mfumo wa ukusanyaji wa ada na uondoshaji taka ngumu wa halmashauri ya mji wa Babati ambapo imebaini mianya ya rushwa ikiwemo uwezo mdogo wa halmashauri kumudu jukumu la uondoshaji wa taka ikiwemo taka ngumu.

Akizungumza katika warsha iliyowakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo watendaji wa kata na mitaa ya halmashauri ya mji wa Babati pamoja na mkurugenzi wa halmashauri hiyo mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Manyara Bahati Haule amesema baada ya uchambuzi wa mfumo huo TAKUKURU imetoa matokeo na mapendekezo yatakayojadiliwa ili kupata muafaka wa kuondokana na mianya hiyo ya Rushwa.

Sauti ya mkuu wa TAKUKURU mkoa Wa Manyara Bahati Haule

Haule amesema uondoshaji wa taka ngumu ni jambo la kisheria, kiafya na kimaendeleo na usipofanyika kwa ufanisi unaweza kusababisha athari za kiafya pamoja na kiuchumi kwa wananchi.Aidha amesema ongezeko la idadi ya watu na kukua kwa shughuli za kiuchumi kumesababisha ongezeko la uzalishaji wa taka ngumu ambapo kutokana na gharama za uondoshaji wa taka kuwa kubwa mamlaka ya usimamizi zimeshindwa kusimamia na kudhibiti taka na kusababisha taka kuwa nyingi katika maeneo yasiyo rasmi.

Sauti ya Mkuu wa TAKUKURU Manyara