FM Manyara

Burunge WMA na mbinu mpya migogoro ya wananchi, wanyamapori

20 March 2025, 1:04 pm

Mkuu wa Wilaya ya Babati Emmanuela Kaganda amefurahishwa na mbinu ambayo imetumiwa na viongozi wa Jumuiya ya hifadhi ya wanyamapori ya Burunge ya kugawa mahindi ili kupunguza migogoro kati ya wananchi na wanyamapori

Na Mzidalfa Zaid

Jumuiya ya hifadhi ya wanyamapori Burunge, imegawa mahindi zaidi ya gunia 300 kwa vijiji 10 vinavyounda jumuiya hiyo kwa ajili ya kuwapelekea wanafunzi wa shule za msingi zinazopatikana katika jumuiya hiyo lengo ikiwa ni kupunguza migogoro kati ya wanyamapori na binadamu.

Akiongea katika hafla fupi ya kukabidhi mahindi hayo mkuu wa wilaya ya Babati Emmanuela Kaganda ameipongeza jumuiya hiyo kwa kuwa wabunifu kwani itapunguza changamoto ya wananchi kulalamika mazao yao kuharibiwa na wanyama  ambapo amewataka watendaji kuhakikisha wanasimamia zoezi hilo la ugawaji mahindi mashuleni.

sauti ya mkuu wa wilaya ya Babati Emmanuela Kaganda

Kwa upande wake katibu wa jumuiya ya hifadhi ya Burunge Benson Mwaise amesema lengo la kugawa  mahindi hayo ni kutokana na kuongezeka kwa changamoto ya wanyama kuharibu mazao hivyo wameandaa mpango huu ili kupunguza changamoto hiyo.

sauti katibu wa jumuiya ya hifadhi ya Burunge Benson Mwaise

Baadhi ya madiwani pamoja na wenyeviti wa vijiji vinavyounda jumuiya hiyo wameishukuru jumuiya ya hifadhi ya Burunge kwa kuendelea kuimarisha jumuiya hiyo ambapo wamesema wataendelea kutunza uhifadhi.

sauti ya madiwani pamoja na wenyeviti wa vijiji