FM Manyara

TPF-NET watoa mafunzo kwa askari wanawake

7 March 2025, 11:54 pm

Mtandao wa Polisi wanawake mkoa wa Manyara (TPF-NET ) wametoa mafunzo kwa askari wanawake

Na Angel Munuo

Mtandao wa Polisi wanawake mkoa wa Manyara (TPF-NET ) wametoa mafunzo kwa askari wanawake ambayo yatawasaidia kupambana na ukatili wa kijinsia pamoja na afya ya akili ikiwa ni kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.

Mrakibu mwandamizi Amina Kahando ambaye ni mwenyekiti wa mtandao wa Polisi wanawake mkoa wa Manyara amesema Katika kuadhimisha siku ya mwanamke wameweza kuwasaidia baadhi ya wanawake ambao walikua na uhitaji wa kuwa msaada wa vitu mbali mbali ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Sauti yaMrakibu mwandamizi Amina Kahando

Aidha Kahando amesema sambamba na maadhimisho haya watatoa Elimu kwa mtandao wa Polisi wanawake ya jinsi ya kukabiliana na matatizo ya afya akili pamoja na namna ya kupambana naukatili wa kijinsia.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Babati Emanuela Kaganda ambaye alikuwa mgeni rasmi amewataka wanawake kuwa waadilifu KATIKA majukumu yao ya kazi ili kuendelea kuaminiwa Kama wanawake kwa kufanya kazi kwa bidii weledi na uadilifu. Kaganda amewapongeza mtandao wa polisi wanawake kwa kutoa elimu kwa askari kwa kuwapatia elimu mbali mbali.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Babati Emanuela Kaganda