FM Manyara

ahukumiwa kifungo cha nje kwa kuuwa bila kukusudia.

5 February 2025, 10:06 pm

Jengo la Mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Manyara

Na George Augustino

MAHAKAMA KUU YA TANZANIA KANDA YA MANYARA IMEMHUKUMU NANGAI SAMWELI GWANDU (25) MKAZI WA KIJIJI CHA TUMATI WILAYANI MBULU MKOANI MANYARA KUTUMIKIA ADHABU YA KIFUNGO CHA NJE MIAKA MIWILI NA MIEZI MITANO KWA KOSA LA MAUAJI YA FABIANO JOHN  (27) BILA KUKUSUDIA.

AWALI AKISOMA MASHATAKA YANAYOMKABILI MTUHUMIWA MBELE YA JAJI MKUU WA MAHAKAMA HIYO DEVOTHA KAMZOLA  WAKILI WA JAMHURI ROSE KAYOMBO AMESEMA MTUHUMIWA ALITENDA KOSA HILO OCTOBER 10 MWAKA JANA 2024 KWA KUMCHOMA FABIANO KITU CHENYE NCHA KALI  KATIKA MAENEO MBALIMBALI YA MWILI WAKE KISHA KUKIMBIA KUSIKOJULIKANA.

WAKILI ROSE AMESEMA BAADA YA TUKIO HILO FABIANO ALIKIMBIZWA KATIKA KITUO CHA AFYA CHA DONGOBESHI KISHA KUPEWA RUFAA YA KWENDA KATIKA HOSPITALI YA HYDOM AMBAPO ALIFARIKI DUNIA KUTOKANA NA MAJERAHA ALIYOYAPATA KWENYE SEHEMU YA UBAVU NA KIFUANI  NA OCTOBA 16 MTUHUMIWA ALIKAMATWA NA KUFIKISHWA KATIKA KITUO  CHA POLISI CHA DONGOBESH NA BAADA YA KUHOJIWA ALIKIRI KUTENDA KOSA HILO.

KWA UPANDE WAKE WAKILI WA UTETEZI TADEY LISTER AMEIOMBA MAHAKAMA KUZINGATIA KUWA MAREHEMU NDIE ALIYEANZISHA UGOMVI NA HALI YA AFYA YA MTUHUMIWA HIVYO MAHAKAMA IMUACHIE HURU MTUHUMIWA KWANI AMESHAJUTIA KOSA ALILOLITENDA BAADA YA KUKAA MAHABUSU KWA MIEZI MITATU MPAKA SASA.

AIDHA
BAADA YA MTUHUMIWA KUFIKISHWA MAHAKAMANI NA KUHOJIWA NA JAJI DEVOTHA KAMZOLA MTUHUMIWA ALIKIRI PIA KOSA NA JAJI KUSIKILIZA UTETEZI WA MAWAKILI WA PANDE ZOTE MBILI MAHAKAMA ILIBAINI MTUHUMIWA ALITENDA KOSA HILO BILA KUKUSUDIA NA KUMHUKUMU KIFUNGO CHA NJE KUTUMIKIA ADHABU MIAKA MIWILI NA MIEZI MITANO .