FM Manyara

TAKUKURU yawaonya wala rushwa kuelekea uchaguzi mkuu

8 January 2025, 1:32 pm

Picha ya mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Manyara Bahati Haule

Kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika mwaka huu, mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Manyara Bahati Haule amesema wameandaa mbinu nyingi za kudhibiti vitendo vya rushwa katika uchaguzi mkuu.

Na Mzidalfa Zaid

Tanzania ikiwa inatarajia kufanya uchaguzi mkuu mwaka huu, Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU mkoa wa Manyara, imesema imejipanga kudhibiti vitendo vya rushwa katika uchaguzi huo na kuhakisha wananchi wanamchagua kiongozi  bora.

Hayo yameelezwa na mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Manyara Bahati Haule wakati akiongea na fm Manyara, amesema kufuatia uchaguzi wa kuwachagua wabunge, madiwani na rais, TAKUKURU itakuwa bega kwa bega na wala rushwa wote kwa kutoawaachia nafasi ya kutoa rushwa na watakaobainika watachukuliwa hatua za kisheria.

sauti ya mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Manyara Bahati Haule

Amewataka wananchi kumchagua kiongozi bora na sio bora kiongozi na Taasisi hiyo imeweka mikakati ya kisayansi ya kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa uwazi na haki, hivyo kila mtu atimize wajibu wake na afaate sheria zilizowekwa za uchaguzi.

Aidha, amesema kwa uchaguzi wa serikali za mitaa uliopita , walipata malalamiko ya ukiukwaji wa taratibu ndani ya  vyama ambapo Taasisi hiyo iliingilia kati na kuvitaka vyama husika kufuata utaratibu kwa mujibu wa vyama vyao.