FM Manyara

TAKUKURU Manyara kuendeleza mapambano ya rushwa 2025

3 January 2025, 5:42 pm

picha ya mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Manyara Bahati Haule

mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Manyara Bahati Haule amesema wataendelea kutoa elimu kwa wananchi kupitia TAKUKURU rafiki, lengo ikiwa ni kuitoa TAKUKURU ofisini na kuwafikia wananchi.

Na Mzidalfa Zaid

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU mkoa wa Manyara, imesema kwa mwaka 2025 imejiwekea mipango ya kupambana na vitendo vya rushwa pamoja na kusimamia miradi yote ya serikali kwa kuhakikisha fedha zote za serikali zinatumika kwa usahihi.

Hayo yameelezwa leo na mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Manyara Bahati Haule wakati akiongea na Fm Manyara iliyomtembelea ofisini kwake  na kuzungumzia mipango ya TAKUKURU katika kupambana na vitendo  vya rushwa kwa kipindi hiki cha mwaka 2025.

sauti ya mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Manyara Bahati Haule

Amesema wataendelea kutoa elimu kwa wananchi kupitia TAKUKURU rafiki, lengo ikiwa ni kuitoa TAKUKURU ofisini na kuwafikia wananchi kwenye kata zote za mkoa wa Manyara na kusikiliza kero zote na kuzipatia ufumbuzi.

Haule amesema katika mapambano ya rushwa, wametembelea shule zote pamoja na vyuo vya mkoa wa Manyara na kuanzisha klabu  za wapinga rushwa ambazo zina weka ushindani kwa kuweka  mada zinazohusu madhara ya rushwa.

Aidha, amesema mwaka 2025 ni mwaka wa uchaguzi mkuu, hivyo TAKUKURU imejipanga kuhakikisha inadhibiti rushwa katika kipindi chote kabla,wakati  na baada ya uchaguzi mkuu.