DC Kaganda azitaka taasisi zisizoshiriki maadhimisho ya Uhuru kutoa maelezo
9 December 2024, 5:38 pm
Mkuu wa wilaya ya Babati Emanuela Kaganda amesema kitendo cha Taasisi ambazo hazikushiriki katika sherehe za maadhimisho ya miaka 63 ya uhuru ni ukosefu wa uzalendo na kushindwa kutambua umuhimu wa siku hiyo ya kitaifa.
Na Mzidalfa Zaid
Mkuu wa wilaya ya Babati, Emmanuela Kaganda amezitaka Taasisi zote za serikali ambazo hazijahudhuria kwenye sherehe za miaka 63 ya uhuru wa Tanganyika, zilizofanyika leo December 9 2024 mkoani Manyara kuwasilisha maelezo ya maandishi yakieleza sababu za kutokushiriki.
Kaganda metoa maagizo hayo alipokuwa akimwakilisha mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga wakati akifungua mdahalo maalum kuhusu uhuru, amesema kitendo cha Taasisi hizo kutokuonekana katika sherehe hizo ni ukosefu wa uzalendo na kushindwa kutambua umuhimu wa siku hiyo ya kitaifa.
Katika madhimisho hayo mkuu huyo wa wilaya amewaongoza wananchi pamoja na vongozi mbalimbali kwa kupanda miti, kufanya mazoezi pamoja na kuwatembelea wagonjwa katika hospital ya halmashauri ya mji wa babati.
Aidha, miaka 63 ya uhuru wa Tanzania imeadhimishwa leo December 9 2024 kwa ngazi za mikoa na wilaya na kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘uongozi madhubuti na ushirikishwaji wa wananchi ni msingi wa maendeleo yetu’.