Babati wabuni mbinu mpya kuhamasisha wananchi kupiga kura
23 November 2024, 8:31 pm
Mkuu wa wilaya ya Babati Emanuela Kaganda amewataka wananchi wote wa wilaya ya Babati kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura kuwachagua viongozi wanaofaa kuongoza mitaa yao, uchaguzi utakao fanyika novema 27 mwaka huu.
Na Mzidalfa Zaid
Kaganda ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wananchi wa wilaya hiyo walioshiriki michezo iliyoandaliwa na ofisi yamkuu wa wilaya ya Babati kwa aajili ya kuhamasisha wananchi kupiga kura siku ya uchaguzi wa serikali za mitaa.
Kwa upande wake mkuu wa Takukuru mkoa wa Manyara Bahati Haule amewataka wananchi wa wilaya hiyo kuacha kupokea rushwa zinazotolewa na wagombea ili wawachague siku ya kupiga kura nakusema kitendo hicho ni kinyume cha kanuni za sheria za nchi.
Aidha, afisa uchaguzi halmashauri ya mji wa Babati Bashan Kinyunyu, amewataka wananchi kuzingatia taratibu zote za upigaji kura ili kuepuka changamoto ya za kura kuharibika.