FM Manyara

Takukuru Manyara kukutana na  vyama vya siasa

20 November 2024, 12:53 pm

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Takukuru mkoa wa Manyara kesho Nov 21,2024 inatarajia kukutana na viongozi wa vyama vya siasa au wadau wa vyama vya siasa vinvyoshiriki uchaguzi .

Na Mzidalfa Zaid

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Takukuru mkoa wa Manyara kesho Nov 21,2024 inatarajia kukutana na viongozi wa vyama vya siasa au wadau wa vyama vya siasa vinvyoshiriki uchaguzi katika mkoa wa Manyara ili kuwapa elimu inayohusu madhara ya rushwa.

Kaimu  mkuu wa Takukuru mkoa wa Manyara Bahati Haule, ameyasema hayo leo wakati akiongea na fm Manyara, amesema katika mkutano huo Takukuru itatoa elimu hiyo  kwa vyama hivyo vya siasa kwakua vina wajibu wa kutoa taarifa wanapooona viashiria vya rushwa.

sauti ya Kaimu  mkuu wa Takukuru mkoa wa Manyara Bahati Haule

Amesema vyama vya siasa vina jukumu la kulinda misingi ya amani,utulivu na mshikamano wa taifa hivyo kupitia mikutano yao wanapaswa kufanya kampeini za kistaarabu ambazo hazitaleta mtafaruku katika jamii.

Aidha,Hauli  amesema Takukuru itamchukulia hatua za kisheria  mtu yeyote atakaekutwa na hatia za kutoa au kupokea rushwa katika kipindi hiki cha uchaguzi kwakua  itapelekea kuchaguliwa kiogozi ambae sio muadilifu.

sauti ya Kaimu  mkuu wa Takukuru mkoa wa Manyara Bahati Haule