FM Manyara

Takukuru Manyara yawataka wananchi kutorubuniwa

19 November 2024, 3:47 pm

Katika kipindi hiki cha uchaguzi, Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU)mkoa wa Manyara imewataka wananchi na wadau wote wa uchaguzi, kuchagua viongozi waadilifu.

Na Mzidalfa Zaid

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU)mkoa wa Manyara imewataka wananchi na wadau wote wa uchaguzi, kuchagua kiongozi bora bila kushawishiwa, kurubuniwa, kuhongwa , kuahidiwa au kutoa au  kupokea rushwa kwakua  kufanya hivyo ni ukiukwaji wa maadili.

Wito huo umetolewa leo na kaim mkuu wa Takukuru mkoa wa Manyara Bahati Haule, alipokuwa akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake akitoa taarifa ya miezi mitatu ya kuanzia mwezi Julay hadi September ambapo ametumia  nafasi hiyo kutoa wito  kwa wananchi  katika kipindi hiki cha uchaguzi wa serikali za mitaa.

amemtaka msimamizi wa uchaguzi kufuata sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi na amewaasa wagombea kufanya kampeini kwa kuelezea sera zao za chama bila kutoa rushwa nakuwataka  wananchi kutoa taarifa watakapobaini kuna viashiria vya kutoa au kupokea rushwa.

sauti ya kaim mkuu wa Takukuru mkoa wa Manyara Bahati Haule

Aidha, amesema takukuru mkoa wa manyara imejipanga kudhibiti vitendo vya rushwa kabla, wakati na baada ya uchaguzi na hatua stahiki zitachukuliwa dhidi ya wagombea na wananchi watakaojihuisha na vitendo vya rushwa.