TRA Manyara yavuka lengo la ukusanyaji kodi
25 October 2024, 8:48 pm
Mamlaka ya mapato TanzaniaTRA mkoa wa Manyara Kwa mwaka 2023,2024 wamefanikiwa kuvuka lengo kwa kukusanya kodi kwa asilimia miamoja na kumi na moja na hii imetokana na baada ya kuwafikia watu kwa kutoa elimu .
Na Mzidalfa Zaid
Mamlaka ya mapato TanzaniaTRA mkoa wa Manyara imeanzisha mfumo uitwayo (TRA mtaani kwako ulipo tupo )ambayo wanawaafata wafanyabiashara kwenye maeneo yao ili kuwasogezea huduma karibu na wanaanchi.
Hayo yameelezwa leo na meneja wa mamlaka ya mapato Tanzania Tra mkoa wa Manyara Alex Katundu wakati akiongea na waandishi wa habari katika banda la TRA lililoko katika maonesho ya Manyara tanzanite trade fair yanayoendelea katika viwanja wa stend ya zamani.
Aidha, katika hatua nyingine Katundu amesema kwa mwaka 2023,2024 wamefanikiwa kuvuka lengo kwa kukusanya kodi kwa asilimia miamoja na kumi na moja na hii imetokana na baada ya kuwafikia watu kwa kutoa elimu .