FM Manyara

 DC Babati atumia mbinu wananchi kujiandikisha

15 October 2024, 5:33 pm

Wakati  zoezi la uandikishaji wa daftari la mkazi unaendelea  nchi nzima Mkuu wa Wilaya ya Babati Emmanuela Kaganda amelazimika kutumia usafiri wa bajaji na pikikpi kuhamasisha wananchi wa Wilaya ya Babati kujitokeza kujiandikisha na kushiriki katika uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajia kuanza Novemba 27, 2024.

Na Mzidalfa Zaid

Mkuu wa Wilaya ya Babati Emmanuela Kaganda leo 0ctober 15 2024 amejiandikisha katika dafatari la mkazi akitumia usafiri wa bajaji kuzunguka maeneo kadhaa ya mji wa Babati kuhamasisha wananchi kujiandikisha.

Kaganda ametumia usafiri huo kuzunguka maeneo kadhaa ya mji wa Babati ikiwa ni pamoja na kwenye vituo vya wasafirishaji kwa njia ya pikipiki na maeneo ya wajasiriamali wadogo kama mama lishe na wafanyabiashara wanaozunguka mji huo.

Akiwa  katika maeneo mbali mbali ya mitaa ya mji wa Babati ametumia fursa hiyo kuelimisha wananchi kuhusu uandikishaji wa daftari la mkazi ili kuwachagua viongozi watakao waletea maendeleo katika maeneo yao

sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Babati Emmanuela Kaganda

Aidha,baadhi ya waendesha pikipiki wamemshukuru  mkuu wa wilaya ya Babati kwa kushirikiana  nao na kumuahidi kuwa wataendelea kufanya hamasa kwa wenzao katika mitaa yao.

sauti ya baadhi ya waendesha pikipiki