Wananchi Babati jiandikisheni daftari la mkazi mapema
11 October 2024, 10:21 pm
Katika kuhakikisha msongamano wa watu unapungua kwa siku za mwisho katika zoezi la kujiandikisha kweye daftari la mkazi, serikali ya halmashauri ya mji wa Babati imewataka wananchi wajitokeze kushiriki zoezi hilo kwa siku za mwanzo ili kuepuka usumbufu wa kukaa kituoni kwa muda mrefu.
Na Mzidlfa Zaid
Wananchi wa halmashauri ya mji wa Babati mkoani Manyara wametakiwa kujitokea kujiandikisha kwenye daftari la mkazi ili kuchagua kiongozi bora wanaofaa kuongoza.
Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Babati Shabani Mpendu amesema hayo baada ya kujiandikisha kwenye daftari la mkazi katika ofisi za mtaa wa Bagara ambapo amewataka wananchi kujitokeza kujiandikisha mapema ili kuendelea na kazi zao kwakua zoezi hilo likitatamatika october 20 na hakutakuwa na muda wa nyongeza.
Amesema kumekuwepo na changamoto ya wannachi kusubiria siku za mwishoni kwenda kujiandikisha hali inayopelekea kuwepo kwa msongamano katika vituo vya kujiandikisha hivyo ni vyema wakajindikisha kwa siku za mwanzo ambazo zinakuwa hazina usumbufu.