FM Manyara
Mwanafunzi aliyepotea mlima Kwaraa apatikana
9 October 2024, 7:36 pm
Mwanafunzi wa kidato cha pili Joel Mariki (14) wa shule ya sekondari Bagara aliyepotea katika mlima Kwaraa ulioko wilayani Babati mkoani Manyara amepatikana.
Na Mzidalfa Zaid
Mwanafunzi huyo yuko katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Manyara ambapo fm Manyara imemtafuta mganga mfawidhi wa hospitali hiyo Catheren Magali , amesema mtoto huyo anaendelea kupata matibabu.
Mwanafunzi huyo alipotea september 14 mwaka huu wakati wakiwa katika matembezi ya kutembelea mlima huo na juhudi mbalimbali zilifanyika za kumtafuta.
Fm Manyara inaendelea na jitihada za kulitafuta jeshi la polisi ili kutoa taarifa kamili juu ya alipokuwa mtoto huyo .