Sillo akabidhi zawadi ya mashine ya kutolea nakala katika shule ya sekondari Matufa
7 October 2024, 9:41 pm
Naibu waziri wa mambo ya ndani Daniel Silo ambae pia ni mbunge wa jimbo la Babati vijijini amekabidhi mashine hiyo baada ya kuwepo kwa changamoto ya upungufu wa vifaa vya shule.
Na Mzidalfa Zaid
Naibu waziri wa mambo ya ndani Daniel Silo ambae pia ni mbunge wa jimbo la Babati vijijini amesema serikali ya awamu ya sita inaendelea kupeleka huduma za kijamii katika kata zinazopatikana kwenye jimbo la Babati vijijini.
Amesema hayo alipokuwa mgeni rasmi katika mahafali ya kidato cha nne katika shule ya sekondari Matufa iliyoko kata ya Magugu wilayani Babati mkoani Manyara ambapo amesema huduma zilizotolewa ni pamoja na maji, umeme, elimu na afya.
Kwa upande wake mkuu wa shule ya sekondari Matufa Herin Mfwangavo, amesema shule yake imekuwa ikifaulisha wanafunzi kila mwaka ambapo amemuomba mbunge huyo kutatua changamoto zinazo ikabili shule hiyo ikiwemo ya kutokuwa na maji katika vyoo vya wanafunzi na walimu.
Akisoma risala kwa niaba ya wahitimu wa darasa la saba mmoja wa wanafunzi hao Nusura Majid amesema shule hiyo inakabiliwa na changamoto ya upungufu wa madarasa na madawati .