Afariki baada ya kubakwa na kutobolewa jicho, Sillo alaani
7 October 2024, 8:34 pm
Serikali yalaani tukio la mwanamke aliyebakwa na kulawitiwa mkoani Manyara ambapo jamii imetakiwa kukemea vitendo hivyo vya kikatili nakuwalea watoto wao katika maadili mazuri.
Na Mzidalfa Zaid
Mwanamke mmoja wa kata ya Magugu mkoani Manyara amefariki baada ya kubakwa na kulawitiwa na vijana pamoja na kumtoboa jicho moja.
Akizungumza na FM Manyara diwani wa viti maalum tarafa Mbugwe Naomi Richard amesema baada ya tukio hilo juhudi alizozifanya ni kuhakikisha vijana waliofanya tukio hilo wanakamatwa.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha Matufa Ramadhani Mangi amesema matukio ya ukatili yameshamiri katika kata hiyo na yanasababishwa na wanachi kushindwa kutoa ushirikiano.
Aidha,naibu waziri wa mambo ya ndani ambae pia ni mbunge wa jimbo la Babati vijijni Daniel Silo amelaani tukio la mwanamke huyo na ameitaka jamii kukemea vitendo hivyo vya kikatili na kuitaka jamii kuwalea watoto wao katika maadili mazuri.