NEC: Simanjiro, Kiteto, Mbulu boresheni taarifa katika daftari la mpiga kura
19 September 2024, 5:46 pm
Tume huru ya taifa ya uchaguzi imewataka wananchi kujitokeza kuboresha taarifa zao katika daftari la kudumu la wapiga kura ili kumchagua kiongozi wanaemtaka.
Na Mzidalfa Zaid
Wananchi wa wilaya za Simanjiro, Kiteto na Mbulu zilizoko mkoani Manyara wametakiwa kujitokeza kuboresha taarifa zao katika daftari la kudumu la mpiga kura ili wapate kadi ya mpiga kura na kushiriki uchaguzi mdogo na uchaguzi mkuuu.
Hayo yamesemwa leo na mkurugenzi wa tume huru ya taifa ya uchaguzi ofisi ya Zanzibar Adam Juma Mkina alipokuwa akiongea na fm Manyara, amesema watu wenye sifa ya kupiga kura ni wenye miaka 18 na kuendelea au watakaotimiza miaka hiyo mwakani.
Amesema zoezi hilo linawahusu ambao hawakuwahi kujiandikisha, waliopoteza kadi ya mpiga kura,waliohama eno moja kwenda jingine pamoja na wanaotaka kuboresha taarifa zao ambapo amesema zoezi hilo linatarajia kuanza september 25 hadi october 1.
Aidha,amewataka wananchi wa wilaya nyingine ambao hawakuhakiki taarifa zao kwa awamu ya kwanza kutokana na sababu mbali mbali wasubiri awamu ya pili ambayo itatolewa na tume.