FM Manyara

Bilionea Mulokozi ajitokeza daftari la kudumu la wapiga kura

September 7, 2024, 6:40 pm

picha ya Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya kuzalisha vinywaji changamshi ya Mati Super Brands Limited  David Mulokozi

Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya kuzalisha vinywaji changamshi ya Mati super brands limited  David Mulokozi amejitokeza kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la Wapiga kura.

Na mwandishi wetu Mzidalfa Zaid

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya kuzalisha vinywaji changamshi ya Mati Super Brands Limited  David Mulokozi amejitokeza kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la Wapiga kura katika kituo Cha Bagara Sekondari  Wilayani Babati Mkoani Manyara huku akieleza kufurahishwa na zoezi hilo linaloendeshwa kwa ufanisi mkubwa na Tume Huru ya uchaguzi na kuwataka wakazi wa mkoa huo kujitokeza kwa wingi.

Mulokozi amesema zoezi hilo linafanyika kwa utaratibu mzuri ambao unamuwezesha kila mwananchi kujiandikisha na kuendelea na shughuli za uzalishaji mali bila kuathiri ratiba zao za kila siku.

sauti ya Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya kuzalisha vinywaji changamshi ya Mati Super Brands Limited  David Mulokozi

Mulokozi amewataka vijana  na wakazi wa mkoa huo kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kujindikisha kwani zoezi hilo halichukui muda na hakuna foleni.

Nao baadhi ya wananchi ambao wanaendelea kujitokeza kuboresha taarifa zao katika vituo mbalimbali mkoni Manyara wamewahimiza wananchi ambao hawajaboresha taarifa zao wafike kwenye vituo vilivyo karibu nao ili wapate haki ya kumchagua kiongozi wanaemuhitaji.

sauti za wananchi mkoani Manyara