Polisi kufanya uchunguzi kifo cha dereva wa Mtei express
5 September 2024, 7:06 pm
Kutokana na kifo cha dereva wa basi la Mtei express Iddi Salehe kupigwa hadi kuuwawa na dereva wa lori, jeshi hilo limesema linaendelea na uchuguzi wa kifo hicho ili mtuhumiwa afikishwe mahakamani.
Na Mzidalfa Zaid
Jeshi la polisi mkoani Manyara limesema linaendelea kufanya uchunguzi wa tukio la dereva wa basi la mtei aliyeuwawa kikatili na dereva wa lori kutoka Rwanda kwa kupigwa na kitu kizito.
Hayo yameelezwa na kamanda wa jeshi la polisi mkoani Manyara Ahmed Makarani wakati akiongea na vyombo vya habari , amesema tukio hilo limetokea september 2 mwaka huu .
Aidha, amesema mtuhumiwa wa tukio hilo anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Manyara na atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili za mauaji dereva huyo.