Twange akabidhi ofisi kwa DC mpya
5 September 2024, 6:40 pm
Baada ya Aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Babati Lazaro Twange kukabidhi ofisi kwa mkuu mpya wa wilaya ya Babati ,amezishukuru taasisi zote zilizopo chini ya ofisi hiyo kwa kumuonyesha ushirikiano katika utendaji wa kazi wakati wote alipoKuwa akifanyakazi katika wilaya ya Babati
Na George Augustino
Aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Babati mkoani Manyara Lazaro Twange leo September amekabidhi ofisi kwa mkuu wa wilaya mpya ya Babati Emanuela Kaganda aliyetokea tokea wilaya ya Arumeru mkoani Arusha. Akizungumza wakati wa makabidhiano ya ofisi Twange amezishukuru taasisi zote zilizopo chini ya ofisi hiyo kwa kumuonyesha ushirikiano katika utendaji wa kazi wakati wote alipokuwa akifanyakazi katika wilaya ya Babati ambapo amemhakikishia mkuu wa wilaya mpya ushirikiano mzuri kutoka kwa wakuu waidara na taasisi zote za ofisi yake.
Kwa upande wake mkuu mpya wa wilaya ya Babati Emmanuela Kaganda amemshukuru rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr Samia Suluhu Hassani kwa kuendelea kuwaamini na kuwapa nafasi ya kuwa wasaidizi wake katika kazi na amewahakikishia viongozi wote na watendaji waliopo katika ofisi hiyo ya mkuu wa wilaya ushirikiano mzuri katika utendaji wa kazi.
Aidha, Twange ameagwa rasmi leo ambapo amehamishiwa katika wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro.