FM Manyara

Zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu kufanyika Manyara

26 August 2024, 7:45 pm

Tume huru ya taifa ya uchaguzi imewataka wadau mbali kuhamasisha jamii kujiandikisha kwenye daftri la kudumu la mpiga kura.

Na Mzidalfa Zaid

Wadau wa uchaguzi wa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura mkoani Manyara wametakiwa kuielimisha jamii kuacha tabia ya kujiandikisha zaidi ya mara moja kwani kufanya hivyo  ni kosa kisheria.

Wito huo umetolewa na mjumbe wa tume ya taifa ya uchaguzi Asina Omar ambae alikuwa mgeni rasmi katika mkutano wa tume na wadau wa uchaguzi uliofanyika katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Manyara, amesema ni kosa kisheria mwananchi kujiandikisha zaidi ya mara moja ambapo pia amewataka wadau hao kuwamasisha wananchi kujiandikisha na kuboresha taarifa zao.

sauti ya mjumbe wa tume ya taifa ya uchaguzi Asina Omar

Kwa upande wake mwakilishi wa mkurugenzi mkuu wa uchaguzi Givness Aswile amesema mkoa wa Manyara unatarajia  kuwa na wapiga kura milioni moja , arobaini na moja elf, miatatu themanini na tisa.

sauti ya mwakilishi wa mkurugenzi mkuu wa uchaguzi Givness Aswile

Nao baadhi ya washiriki wa mkutano huo , wamesema watafikisha elimu ambayo wameipata kwenye jamii inayowazunguka huku wakiomba serikali kusimamia vizuri zoezi hilo.

sauti ya baadhi ya washiriki wa mkutano huo