Madhara yatokanayo na matumizi ya dawa za kulevya yatajwa
20 August 2024, 4:29 pm
Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya Kanda ya Kaskazini yawataka vijana kuacha kutumia dawa za kulevya .
Na Mzidalfa Zaid
Vijana mkoani Manyara na Kanda ya Kaskazini kwa ujumla, wametakiwa kuacha kutumia dawa za kulevya kwa kuwa zinaathiri utendaji kazi pamoja na kufanya matukio yasiyo sahihi.
Hayo yameelezwa leo na afisa elimu jamii kutoka mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya Kanda ya Kaskazini Abdlatifu Said wakati akiongea na FM Manyara, amesema vijana wengi wanaathirika na dawa za kulevya.
Kwa upande wake mkuu wa dawati la elimu kwa umma (TAKUKURU) mkoani Manyara Hamis Ally ameitaka jamii kuacha kupokea au kutoa rushwa huku akiwaasa wananchi kutoa taarifa kwa taasisi hiyo pale wanapobaini viashiria vya rushwa.
Aidha, amesema katika kipindi hiki cha uchaguzi wananchi wasipokee rushwa kwani kutapelekea wananchi kumchagua kiongozi asiye na sifa za kuongoza.