FM Manyara

Klabu ya waandishi wa habari Manyara yapongezwa

August 9, 2024, 6:02 pm

Baada ya balozi Sharlotta Ozaki Mercias kutembelea klabu mbalimbali na za waandishi wa habari katika mikoa tofauti, amesema mkoa wa Manyara umekuwa mfano mzuri kutokana na ushirikiano uliopo baina ya waandishi wa habari na jeshi la polisi.

Na Mzidalfa Zaid

Balozi wa Sweden nchini Tanzania Sharlotta Ozaki Mercias amekipongeza chama cha waandishi wa habari mkoani Manyara kwa kufanya kazi za kijamii ikiwemo kuibua matukio mbalimbali pamoja na kukemea vitendo vya kikatili.

Mercias ameyasema hayo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari katika ofisi  za chama cha waandishi wa habari zilizoko mkoani Manyara, amesema ametembelea klabu mbalimbali za waandishi wa habari katika mikoa tofauti lakini mkoa wa Manyara umekuwa mfano mzuri kutokana na ushirikiano uliopo baina ya waandishi wa habari na jeshi la polisi.

Sauti ya Balozi wa Sweden nchini Tanzania

Kwa upande wake mkurugenzi wa muungano wa klabu za vyama vya waandishi wa habari Tanzania Keneth Simbaya amewaasa wanahabari  kuendelea kuripoti habari zenye kuisaidia jamii pamoja na serikali kwa ujumla.

Sauti ya Mkurugenzi wa Klabu za vyama vya waandishi wa habari Tanzania

Aidha,mratibu wa chama cha waandishi wa habari mkoani Manyara Goodluck Sendula,amesema chama cha waandishi wa habari mkoa wa Manyara kinaendelea na mkakati wa kutembelea vituo mbalimbali vya radio ili kuongeza idadi ya wanachama kwa ajili ya kuendelea kukijenga chama hicho na akielezea namna chama hicho kinavyosaidia kupinga ukatili wa kijinsia.

sauti ya mratibu wa chama cha waandishi wa habari mkoani Manyara